Na Geofrey Chambua.
Ni ngumu kuongelea udukuzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Urusi KGB ndani na nje ya Uingereza na shirika lake la kijasusi MI6 bila kutaja jina 'Kim Philby'.
Ni nani hasa huyu Kim Philby?, kwanini iwe ni muhimu kama si lazima kumtaja?, ni upi mchango wake ndani ya KGB unaompa heshima hiyo?. Maswali yote haya tutayapatia majibu kadiri tutakavyozidi kumfahamu jasusi huyu hodari wa Kirusi.
Kati ya miaka 1920s-1930s Kim Philby alijiunga na chuo cha Cambridge kilichopo Uingereza akichukua masomo ya Uchumi, taaluma iliyokuwa na mashiko hasa miongoni mwa wakomunisti waliochochewa kwa kiwango kikubwa na falsafa za uchumi za Karl Marx.
Akiwa amebobea ndani ya falsafa za kikomunisti Philby aliwasaidia tabaka la chini la wafanyakazi kupata mahitaji muhimu kama chakula kutokana na anguko la uchumi miaka ya 1930 uliotokana na mdororo wa soko la hisa.
Haukupita muda ujerumani chama cha Nazi kikatwaa madaraka chini ya dikteta Adolf Hitler, hali ya wakomunisti ikazidi kuwa mbaya ndani ya mataifa ya magharibi na hapa ndipo KGB ilipoamua kumsuka na jasusi kijana Kim Philby.
Chini ya KGB Philby alitakiwa kubadili mtazamo kutoka ukomunisti na kuwa mfashisti kwa maslahi ya ukomunisti. Ndani ya ufashisti Philby alijiunga na Anglo-Germany Fellowship na kuwa moja ya vijana walioaminika sana.
Akiwa kama mfashisti Philby aliweza kuonana na viongozi wengi wa kifashisti ikiwa ni pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Vonrbentrap aliyemtuma kwenda kuimarisha ufashisti huko Hispania kazi aliyoifanya vyema hadi kupatiwa medali ya heshima.
Safari ya Philby haikuishia kuwa jasusi wa Urusi ndani ya Nazi bali mwanzoni mwa vita vya pili vya dunia Philby alifanikiwa kupenyeza ndani ya vyombo vya kijasusi vya Uingereza na kupewa mafunzo na shirika la kijasusi la MI6. Mwenendo huu wa Kim Philby ulianza kuwapa wasiwasi mabosi wake ndani ya KGB ikiwa ni pamoja na Joseph Stalin mwenyewe.
Akiwa ndani ya MI6 Philby alizidi kulitumia taifa lake la Urusi nyaraka nyeti za vita na mipango ya Uingereza taarifa ambazo ziliisaidia Urusi kwa kiwango kikubwa kipindi cha vita ya dunia, miongoni mwa nyaraka hizo ni pamoja na opeesheni citydel na mpango wa Uingereza kuivamia Urusi baada ya kuipiga Ujerumani.
Baada ya vita vya dunia vya pili kumalizika, Philby alizidi kupanda ngazi na kupewa medali ya excellent Order na malkia wa Uingereza. Huku vigogo wa MI6 wakimuingiza kwenye orodha ya warithi wa kiti cha mkuu wa MI6 bila kujua kuwa wanajikaanga wenyewe.
Hatua hii ya kumfikiria Phliby kama mtarajiwa wa kuiongoza MI6 ni moja ya vitu vinavyomtanabaisha jasusi huyu katika hali ya kipekee.
Akiwa ni KGB ndani ya MI6 Philby aliweza kuwaokoa majasusi wenzake wa kirusi waliokuwa wakifanya ujasusi uingereza na kushukiwa na Uingereza.
Lakini walimwengu walisema hakuna marefu yasiyo na mwisho hatimaye Uingereza ilianza kumshuku Philby kuwa mchuuzi kwa kuwa Philby alikuwa tayari anaijua vyema 'system' ya Uingereza aliweza kuepuka mtego huo hatari huku akisafishwa kwenye vyombo vya habari.
1962 kwa mara ya pili Kim Philby alishukiwa tena kuwa ni jasusi wa urusi baada ya jasusi mwenzake wa kirusi kumtaja kama jasusi wa urusi awamu hii kukawa na ushahidi wa wazi, wakati wa kuhojiwa Kim Philby kwa umakini mkubwa alikubali kuwa alikuwa ni jasusi wa Urusi hadi mwaka 1946 na baada ya vita alikuwa mtu huru, mwanzo MI6 ilikubaliana na utetezi huo wa Philby na kumuachia huru.
Ni mwanya huu ndio ulioweza kuidhihirishia Uingereza kuwa walikuwa chini ya KGB bila kujijua kwani Philby aliamua kutoroka na kukimbilia Urusi ambapo alipokewa kwa heshima kama shujaa wa taifa hilo.
Akiwa Urusi Kim Philby alifundisha katika shule ya majasusi huko Moscow hadi umauti ulipomfika. Inasemekana kuwa unywaji wa pombe uliopitiliza ulichangia kifo cha jasusi huyu hodari.
Comments
Post a Comment