MOTO MKUBWA UMETEKETEZA SOKO LA NGUO MBEYA

Moto mkubwa umetokea jijini mbeya usiku wa saa 3 15/8/2017 katika soko la Nguo na kuteketeza maduka ya nguo soko la Sido katika Mtaa wa Mwanjela chanzo cha moto huo hakijahamika
Watu walioshuhudia tukio hilo, wamesema moto huo ulianza jana majira ya saa 3:15 asubuhi na kusambaa kwa kasi katika vibanda vya wafanyabiashara, hali iliyowaweka katika wakati mgumu askari wa Kikosi cha Zimamoto walioshindwa kuudhibiti moto huo mkubwa.

Askari wa Kikosi cha Zimamoto waliowahi kufika katika eneo la tukio wakiwa na magari mawili, lakini walishindwa kuufikia moto huo ambao ulianzia katikati ya soko kutokana na 

miundombinu mibovu ya barabara ambayo hairuhusu gari kuingia ndani ya soko.
Aidha, shughuli za uokoaji wa mali ziliingia dosari, baada ya askari wa Jeshi la Polisi waliochelewa kufika katika eneo la tukio kuamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vibaka
Changamoto ni miundombinu na umbali kwa nchi na kwa mbeya gari la zima moto llinalotumika ni gari linalotoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa songwe ambapo ni mbali kigogo katika jiji la mbeya.
Wafanyabiashara biashara wamekubwa na taharuki na kuokoa mali zao kwa ukubwa wa moto   
Na kwa mujibu wa wenyeji wa mkoa wa mbeya wameeleza tukio la moto ni la mara kutokea na katika soko hilo ni mara ya pili lakini moto huu ni mkubwa kulinganisha na matukio ya moto ambayo yameshawahi kutokea.
 Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Anaclet Malindisa, alisema moto huo ni mkubwa ambao haujawahi kutokea jijini Mbeya na kwamba umesababisha uharibifu mkubwa wa mali za wafanyabiashara wa eneo hilo.
Alisema Jeshi la Polisi limejitahidi kulinda amani katika eneo hilo na vurugu zilizotokea zilisababishwa na vijana waliokuwa wakikaidi amri halali ya Polisi ya kuwataka waondoke kwenye eneo hilo kwa sababu za usalama. Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Evance Balama, alisema tukio hilo ni kubwa na la kusikitisha, ambalo limesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara.


Hata hivyo, alisema tukio la moto pamoja na vurugu zilizotokea visihusishwe na siasa kwa kuwa moto umetokea kwa bahati mbaya na vurugu hizo zinatokana na Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wake hawafi kwa janga ambalo lingetokea kama moto huo ungefika kwenye kituo cha mafuta kilicho jirani.
Hili ni soko la tatu kuungua jijini Mbeya. Desemba 2006, Soko Kuu la Mwanjelwa ambalo wafanyabiashara hao walikuwa wakifanyia biashara kabla ya kuhamishiwa eneo la Sido liliteketea kwa moto na Desemba mwaka jana, Soko Kuu la Uhindini pia liliteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabishara.


Comments