- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema serikali imejipanga kuhakikisha inapambana na uhalifu wa aina yoyote ikiwemo makosa ya kimtandao na ugaidi.
Waziri Nchemba ametoa kauli hiyo wakati akiweka jiwe la msingi katika upanuzi wa Shule ya Polisi Moshi upanuzi ambao utawasaidia wanafunzi wa polisi kupata mafunzo ya kukabiliana na njia zote za
uhalifu wa mitandao.
uhalifu wa mitandao.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema suala la usalama ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho uchumi wa nchi unaendelea kukua.
Zaidi ya wanafunzi mia tano wanatarajiwa kupata mafuzo ya kompyuta pamoja na wanafunzi Mia Nane kulala katika mabweni huku ujenzi ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2018.
Comments
Post a Comment