Injini ya ndege ya abiria ya Air France, yaharibika angani



Abiria waliona injini iliyoharibika kupitia dirisha la ndege na wakapiga picha
Image captionAbiria waliona injini iliyoharibika kupitia dirisha la ndege na wakapiga picha
Ndege moja kubwa ya abiria ya AirFrance, muundo wa Airbus 380, imelazimika kutua kwa dharura baada ya injini yake moja kuharibika vibaya, ndege hiyo ikiwa angani.
Ndege hiyo superjumbo ilikuwa njiani kuelekea Los Angeles- Marekani kutoka mji mkuu wa Ufaransa- Paris, ikiwa na zaidi ya abiria 500.
Iliamua kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Goose Bay, mashariki mwa Canada.
Bawa la ndege halikuharibika vibaya, hatua iliyosababisha ndege hiyo kutua uwanjani vyema
Image captionBawa la ndege halikuharibika vibaya, hatua iliyosababisha ndege hiyo kutua uwanjani vyema
Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika kisa hicho, lakini abiria walisalia ndegeni kwa saa kadhaa, baada ya ndege hiyo ya abiria kutua.
Wakati wa kisa hicho, ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 496 na wafanyikazi 24. Hayo ni kwa mjibu wa msemaji wa Air France spokesperson, aliyezungumza na shirika la habari la AFP.
David Rehmar, mekanika wa zamani ambaye alikuwa abiria katika ndege hiyo, ameiambia BBC kuwa, kutokanana na uchunguzi wake, kisa hicho huenda kilitokana na kushindwa kwa feni ya injini ya ndege hiyo.
Njia ya ndege hiyo angani
Image captionNjia ya ndege hiyo angani
Anasema kuwa kulitokea ghafla, baada ya mlio mkubwa kusikika, ambayo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria.

Comments