Mbinu Tata Za Kumfanya Mwanamke Akufukuzie



Awali tuliandika kuhusu mbinu za kumfanya mwanamke akufukuzie. Well, leo tumeamua
kuja na mbinu tata ya kumfanya mwanamke akufukuzie.


Baada ya kufanya majadiliano na paneli yetu ya Nesi Mapenzi, editor wetu mkuu aliidhinisha
 tuiweke wazi mbinu hii tata hata angalau kwa uchache ili iweze kutumika na readers wetu.
 Awali tulishaandika chapisho la kumkontrol mwanamke kama rimoti, kutumia
mbinu ya I.O.U kulala na mwanamke pamoja na mbinu nyingi zaidi ambazo
 tumeziorodhesha kama Sanaa Ya Kutongoza. Hii mbinu tata ya kumfanya
 mwanamke kando na kuwa wanawake wengi wanaikashifu, pia huwa inafanya kazi.

Kama umekua ukifuatilia machapisho yetu unakumbuka kuwa tushaeleza na
kufafanua kuwa katika ubongo wa mwanamke kuna chembechembe za DNA
ambazo zimeandikwa mahususi kumtumikia mwanaume. Hii ndio maana utamkuta
mwanamke nyakati zote za maisha yake huwa anajiweka chini ya mwanamke.
Udhaifu huu ndio wanaume ‘wachache’ huwa wanatumia kumlainisha mwanamke kila wakati.

Ok, kupunguza maelezo yawe mafupi, mbinu zenyewe  tata za kumfanya mwanamke
 akufukuzie ndizo hizi:

#1 Mfanye mwanamke ajihitimishe kwako
Unaweza kumuuliza swali kama “Ni kitu gani ambacho kinakufanya
 unique/tofauti na wengine?”
Ama kumwambia, “Wewe unakaa mdogo sana kiumri kwangu.
 Ni kitu gani ambacho uko nacho ambacho kitaziba pengo hilo?”

Ataanza kukupatia sababu ambazo anajiona kuwa yeye ni unique – kiufupi atakuwa
 akijaribu kujieleza zaidi ili ajipendekeze kwako/ umpende zaidi. Yaani atakuwa
anajaribu kuhakikisha kuwa unaridhika na kila kitu ambacho atakwambia.

Na uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa kadri mwanamke anavyokuwa mrembo
 ndivyo zaidi utakavyohitajika kumfanya ajihitimishe kwako, usiogope kumuuliza
maswali ambayo yatamlazimu ajihitimize kwako. Muulize maswali mazito.
 Muulize maswali ambayo itakuwa ngumu kwake kujihitimu kwako.

Na kitu cha kufurahisha kuhusu wanawake warembo, ni kuwa wamezoea kufukuziwa
 na wanaume kiasi cha kuwa ukianza kuuliza maswali na kujihitimu kwako,
atafall na wewe zaidi. Hii ni kwa sababu hawajazoea kuulizwa maswali kama hayo
. Hawajazoea kuambiwa, “Wewe si mwanamke type yangu.” ama, “Ningekutongoza
 lakini unanikumbusha ndugu yangu wa kike mdogo.”

Pia unapaswa kuhitimisha wanawake kulingana na ladha yako. Labda kwa mfano
 hupendi wanawake wanaovuta sigara, kunywa pombe nk, basi mhitimishe kwa
 kutumia mambo haya. Usimfiche. Mwambie ukweli. Kumwambia mambo kama
 haya kutamfanya ajue vigezo vyako. Unampa challenge na yeye kutaka kutimiza
vigezo vyako. Mbinu hii ni rahisi ya kumuwin kirahisi na kumfanya akufukuzie.

#2 Tumia miondoko ya mwili funge na wazi
Mara ya kwanza unapoongea na mwanamke huwa anaangalia kando. Wewe
 ndie uko wazi, unaongea na yeye, unamwangalia, lakini yeye ameangalia kando kabisa.

Hapo kuna ile hisia ambayo inakuja ndani yako kuwa huyu mwanamke hamakiniki na wewe kabisa.

Well, hapa ndipo unatumia mbinu funge ya kuiga vile ambavyo anafanya yeye.
 Wakati umemuapproach, si lazima umuangalie mzima mzima kwanza, unaweza
kuangalia kiupande. Na akiongea kitu ambacho umependezwa nacho, unaweza\
 kutumia mwondoko wazi kwa kuangalia upande wake. Na akisema kitu ambacho
 hujapenda basi tumia mwondoko funge kwa kuangalia kando.

Mbinu hii hufanya kazi kwa kuchukua atenshen na umakinifu wa mwanamke.
Atamakinika kwa kila neno ambalo atakwambia. Mwishowe itajeuka kuwa ni
yeye ndiye anayekufukuzia na wala si wewe. Mbinu hii pia inampa confidence
 ya kutamka mambo ambayo si rahisi kutamkwa na mwanamke hivihivi.

#3 Tumia toni saidizi iliyovunjwa.
Katu mwanamke hawezi kukufukuzia kama utatumia toni saidizi kama, “Mambo
 waendeleaje?” ambapo sentensi kama hii toni ya sauti inapanda mwishoni. Kama
 vile unauliza swali. Matumizi ya sentensi hizi zitakufanya uonekane mtu mdhaifu,
 mhitaji, na utafanya wanawake wakukimbie.

Lakini ukitumia toni saidizi zilizovunjwa kwa mwanamke kama, “Hey! Njoo hapa!
 Waendeleaje!”  unatoa sauti ya kuamrisha na ya kutoa maelekezo.

Na kwa kuwa uasili wa mwanamke ni kufuata amri, atakujibu kwa kutafuta toni
saidizi ili aweze kujihitimisha kwako.

Atakwambia, “Mmh, jina langu ni Mamito?” huku akitaka umthibitishe.

So, ukimwambia, “Sasa, mpangilio wako ni upi!? kwa toni saidizi iliyovunjwa, atakujibu...

“Mmh, mimi mwanafunzi nasomea...huu ni mwaka wangu wa...”

Kiufupi hapa anajaribu kujieleza zaidi kwako kulingana na vile sauti yako ilivyotoka

#4 Weka nafasi (sukuma)
Unapoongea na mwanamke, hutaki kuona umepalilia maongezi bila mpangilio,
 badala yake huwa unataka nafasi angalau kurudi nyuma kiasi kuyapa maongezi
 yenu nafasi ya kupumua. Unaruhusu kuwe na angalau kimya ndani yake.
 Kimya ambacho kinaenda polepole. Na nafasi ambayo utampa mwanamke
 nafasi ya kujileta kwako ili kuteka atenshen yako.

So mpe mwanamke nafasi ya kujiekeza kwako, na utagundua kuwa mwanamke
anakusaidia pakubwa kuyafanya maongezi yenu yanawiri.

Atafurahi kukupa namba yake ya simu kwa kuwa anakufukuzia.

Atafurahi kukutana na wewe katika deti ya pili.

Na hatakutatiza zile nyakati za mwisho mwisho za kumuomba penzi.

Comments