Mfalme Mswati aongeza mke wa 14


 Mfalme Mswati III  wa Swaziland wiki iliyopita ameongeza idadi ya wanawake aliioa na kufikisha 14, kwa kumuoa msichana wa miaka 19.

Msichana huyo ajulikanaye kwa jina la Siphelele Mashwama ambaye ni mtoto wa mshauri wa baraza la mawaziri nchini Swaziland, Jabulile Mashwama. atakuwa amefikisha idadi ya wanawake 14 wa Mfalme tangia aingie kwenye utawala mwaka 1986.

Kwa mujibu wa gazeti la Maravi Post taarifa za kuoa kwa Mfalme huyo zilithibitishwa na msemaji wa familia hiyo ya kifalme, Hlangabeza Mdluli na kusema kuwa Mfalme Mswati (49) ameoa wiki iliyopita na kwa sasa  yupo na mrembo huyo nchini Marekani kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa.

Msichana huyo alipatikana kwenye sherehe za msimu wa ngoma za asili zijulikanazo kama ‘Umhlanga Annual Reed Dance’ ambapo mamia ya wasichana wenye bikra hujitokeza kujaribu bahati yao ya kuolewa na Mfalme.

Mfalme Mswati kwa sasa ana watoto 13 ambapo binti yake wa kwanza Princess Sikhanyiso ana miaka 23 na wengine ni Sibahle Dlamini, Makhosothando Dlamini, Majaha Dlamini, Tiyandza Dlamini, Sakhizwe Dlamini, Saziwangaye Dlamini, Bandzile Dlamini, Lindaninkosi Dlamini, Mcwasho Dlamini, Temtsimba Dlamini na Temaswati Dlamini.

Comments