- Get link
- X
- Other Apps
Akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, TID amesema sababu inayomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kutokana na mbunge wa sasa kushindwa kulitimizia mahitaji yake jimbo hilo, hivyo atatumia nafasi hiyo kuhakikisha anamng'oa ifikapo 2020, kwa kuwa yeye anafahamu vizuri matatizo ya Kinondoni kutokana na kuwa mzawa wa mahali hapo.
Akiendelea kuzungumzia suala hilo, TID amesema iwapo atapewa dhamana ya kuliongoza jimbo hilo, atahakikisha anatatua matatizo yote yanayowakabili watu wa Kinondoni, likiwemo janga la madawa ya kulevya.
Comments
Post a Comment