Ajali ya treni yauwa 16

Ajali ya treni iliyogongana na basi nchini Urusi imepelekea watu wasiopungua 16 kuuwawa. Wengine kadhaa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali. Bahati hizo zimetangazwa na maafisa wa serikali ya Urusi. Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo, umbali wa kilomita 110 mashariki ya mji mkuu Moscow. Ripoti zinasema ajali imetokea baada ya basi kukiuka njia licha ya taa nyekundu na kukwama baadae katika njia ya reli. Ajali za basi zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara nchini Urusi. Mwishoni mwa mwezi wa agosti watu 17 waliuwawa kusini mwa Urusi, basi iliyokuwa na wafanyakazi wa bandarini ilipoanagukia katika bahari nyeusi.

Comments