AY,FA na Fid Q ‘tumekuja kubadilisha muziki’

Wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, AY , Mwana FA pamoja na Fid Q Ijumaa hii katika kiota cha burudani cha Tips Lounge Mikocheni jijini Dar es salaam wamezindua video yao mpya ya wimbo ‘Upo Hapo?
Shughuli hiyo ambayo ilidhaminiwa na Mkito pamoja na Hennessy ilivutia mashabiki wengi wa muziki baada ya siku chache zilizopita kusambaa picha mtandaoni zikimuonyesha AY akiwa anauza nyama buchani.


Wakizungumza katika uzinduzi huo muda mfupi baada ya kuzindua project hiyo, AY amesema video hiyo mpya inaweza kubadili muolekeo wa muziki nchini Tanzania kutokana na stori yake.


Mwana FA, AY pamoja na Fid Q wakiwa katika uzinduzi huo


“Kukutana sisi watatu ni kazi kubwa kwanza, na hii kazi inakuja kubadili upepo wa muziki wetu ni kama movies kabisa. Kwa hiyo sisi kama sisi tulitafuta muda tukatengeneza kazi halafu baada ya hapo tukasema nilazima tufanye kazi ambayo kila mtu akiiona atasema alichosema AY ni kweli,” alisema AY.


Kuhusu muungano wa kama ni kundi, FA alisema ni vigumu kwa wao kuwa kama kundi kwa sasa kwa kuwa kila mmoja ni msanii mkubwa na tayari wana mambo mengi binafsi wanafanya.


“Huwezi kutengeneza kundi la watu hawa watatu, patachimbika,” alisema FA huku wakicheka kwa pamoja.


Naye Fid Q alisema wao hawawezi kuwa kundi tena kutokana na stori walioitengeneza kwenye video hiyo wa wimbo ‘Upo Hapo’?.


“Huu wimbo wenyewe unajieleza kwamba hatuwezi kuwa kundi, ndani ya kundi kila mtu mbabe sasa sijui kama tunaweza kukaa pamoja kweli ladha tuombewe kwanza, mashabiki tuombeeni” alisema Fid Q.

Comments