Barakah The Prince ajibu ishu ya kumuomba msamaha Alikiba


Msanii wa muziki Bongo Flava, Barakah The Prince amefunguka ishu ya kumuomba msamaha Alikiba.
Barakah The Prince ambaye aliondoka katika label ya RockStar4000 baada ya Alikiba kuwa miongoni mwa mabosi wa label hiyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa wao hawajawahi kugombana hivyo suala la kuomba msamaha halipo.
“Mimi na Alikiba hatuna tatizo, tuna muda tu hatujawasiliana lakini sijawahi kuwa na tatizo naye isipokuwa watu wanaforce mimi kuwa na matatizo naye, inaweza kuwa ni mashabiki, pia watu wake wa karibu” amesema Barakah.
Ameongeza kuwa tangu aondoke RockStar4000  hawajawasiliana na tatizo ni kwamba mara nyingi simu ya Alikiba ikipigwa huwa haipokelewi.

Comments