jeshi la polisi Mkoa wa kipolisi wa TEMEKE linawashikilia watuhumiwa Thelathini na Nne (34) wakiwemo wasichana wadogo ishirini na nane (28) kwa tuhuma za kufanya biashara ya ngono ktk maeneo ya Tandika na Temeke jijini humo.
Pia polisi kwa kushirikiana na raia wameyafungia madanguro yenye vyumba 170 ambavyo vilikuwa vikitumika kwa biashara hiyo.
Watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani tarehe 30/10/2017 siku ya jumatatu kusomewa mashitaka yao yanayowakabili.
#Kwa mkoani #KIGOMA biashara hii imeshamiri kabisa na maeneo tunayajua vijana wanaharibika kwa kweli hasa watoto wakike.
Hivyo nitoe wito kwa wananchi na jeshi la polisi kwenda kuwasaka wale wote wanaojihusisha na biashara ya ngono maana sio nzuri na mwisho wake huwa ni mbaya kabisa.
Comments
Post a Comment