HARMONIZE SINA BEEF NA IDRIS SULTAN


Image result for harmonizeMsanii wa muziki wa Bongo Flava kutoka label ya WCB, Harmonize amesema si kweli kwamba ana beef na Idris Sultan.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shulula’ ameiambia The Playlist ya Times Fm stori za kuwepo beef kati yao huwa zinatengenezwa na baadhi ya watu tu.
“Sina beaf na Idris na sijawahi kuonana naye am tell you, ni stori tu naona watu wanatengeneza kila siku halafu kingine mimi ni mtu wa kusamehe sana haya mtu akiwa amenikosea kabisa naamini kuwa ni binadamu hajakosea, inawezakana hata mimi nakoseaga watu” amesema Harmonize.
Kwa mujibu wa stori zilizokuwa sikizagaa zilidai kuwa wawili hao walikutana usiku wa party ya birthday ya Diamond, ila Idriss alipomsalimu Harmonize hakuitika kitu ambacho amekikanusha vikali.

Comments