
Kimbunga Nate kimesababisha upepo mkali, mvua kubwa na mafuriko kwenye pwani ya Ghuba ya Marekani.
Kimbunga hicho chenye upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 137 kwa sasa, kilitua karibu na mto Mississipi huko Louisiana baada siku ya Jumamosi.
Kikisonga kwenda kaskazini kilitua eneo la Bioloxio huko Mississipi
Louisiana, Mississippi, Alabama na sehemu za jimbo la Florida mapema zilitoa onyo kuhama wakati kukiwa na hofu ya kuongezaka kwa haraka viwango vya maji.
Nate kiliwaua takriban watu 25 huko Nicaragua, Coasra Rica na Honduras.

Kimbunga hicho kisha kikaongeza nguvu hadi kiwango cha kwanza eneo la Saffir-Simpson scale kilipoelekea Marekani.
Wakati Nate kilisonga mbele mitaaa na barabara huko Biloxi vilifurika
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumamosi alitangaza hali ya dharura huko Louisiana, na kuruhusu jimbo hilo kuomba msaada wa serikali kwa maandalizi.
Huko Alabama, gavana wa Republican Kay Ivey, aliwashauri wakaazi katika sehemu zinazokumbwa na upepo mkali kuchukua tahadhari.
Bandari tano zilifungwa kama njia ya kuchukua tahadhari.

Comments
Post a Comment