
Rais Donald Trump na Larry Flynt
Bwana Flynt kupitia tangazo lake alilotoa kwenye gazeti la Washington Post amesema atatoa kiasi cha dola milioni $10 sawa na Tsh bilioni 22 kama zawadi kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa chafu kumuhusu Rais Trump ambazo zitamfanya ang’atuke madarakani.

Tangazo la Larry Flynt
Flynt, amesema kila Mmarekani anawajibu wa kumuondoa madarakani Rais Trump kwani wakichelewa basi taifa hilo litakuwa na machafuko makubwa ya kibaguzi.
“Kumtoa Rais Trump madarakani kitakuwa ni kitendo cha kiungwana, kwani miaka mitatu iliyosalia kuishi nae ni kama safari ya jangwani, hili ni jukumu letu sote wamarekani bado hatujachelewa,“amesema Flynt kwenye Tangazo hilo.
Comments
Post a Comment