Katika dunia ya siku hizi kuna wanawake aina aina nyingi sana. Leo tumeamua kuwaanika hawa wanawake wanaojulikana kama gold digger. Kawaida yao huwa wanajiingiza katika mahusiano na windo lao pasi na mlengwa kujielewa. Mwanaume anayenaswa katika hali hii mara nyingi hawezi kutambua iwapo yuko katika hali ya mahusiano ama kitega uchumi.
Gold digger ni mtu aina gani?Hii ni sampuli ya mwanamke (pia kuna wanaume aina hii) ambaye anatumia mahusiano kama kitega uchumi. hujiingiza katika mahusiano kunufaika kiuchumi. Yeye hana haja na mapenzi. Ilimradi umlipie gharama zote ambazo anahitaji yeye yuko sawa kuendelea na wewe hadi mwisho.
Je huyu mwanamke ana athari gani kwa maisha yako?Ok. Wanaume wengine wangesema hawana tatizo na kuwa na mwanamke aina hii. Kama pesa niko nazo ya nini nilalamike? Mwache azitumie mpaka achoke yeye. Well, hapa Nesi Mapenzi tuna mtizamo tofauti. Mwanamke anayejitokeza kama gold digger huwa anatumia saikolojia kukuteka nyara kiakili na mawazo. Atatumia mbinu fioa za kukuzuzua kiasi cha kuwa kila kitu akitaka utampa bila wewe kufikiria. Na ukikataa ama kama umeishiwa na hela siku moja au nyingine atakunyima kitu ambacho umezoea kupata kutoka kwake. Mfano wa gold digger leo ukimwambia sina pesa za kukununulia simu ya iPhone X, siku ya pili hatopokea simu yako ama mbaya zaidi atakuwekea mgomo baridi usikaribie tunda lake. Upo!? Hebu tuziangalie baadhi ya tabia za huyu mwanamke gold digger.
#1 Anakubaliana na kila kitu. Kuna wanawake wengi ambao huwa wametulia na ni rahisi kukubaliana na wewe lakini kwa hawa magold digger ni tofauti. Wao huwa wepesi sana, na kila kitu utakachowambia huwa wanakuwa wachangamfu kufanya ili wakuridhishe. Hii ni mbinu ambayo wanawake aina hii hutumia kuisimamia akili yako.
#2 Mnafanana kila kitu. Hii ni mbinu nyingine wanaitumia kuisimamia akili yako. Mara ya kwanza kukutana atakwambia kuwa anapenda kila kitu ambacho unapenda. Utajua ukweli wa haya maneno kwa jinsi anavyokujibu. Mfano ukimwambia kitu atakujibu, "Pia mimi."
#3 Anakupa heko kupita kiasi. Kuna wakati mwingine kutoa heko inafikia mahali kunapita kiasi. Mwanamke aina hii utamwona anakusifia kwa kila kitu. Ukifanya jambo flani anakusifia, ukifanya lile anakusifia, hata kupiga mswaki anakwambia, "Leo bebi umeng'ara meno" Hapo jua fika kuwa anauangalia mfuko wako zaidi ya pendo lako.
#4 Anatumia mzigo kama silaha. Hii atahakikisha kuwa ameiweka katika akili yako. Anatumia saikolojia kukuweka katika hali ya kukutunuku. Ukikosa kumfanyia kitu flani kwa mfano kumnunulia kiatu latest, atakunyima kufanya mapenzi na wewe. Lakini pindi utakapomnunulia kile anachohitaji anakupa mzigo wote. Hapa anakuweka hali mbaya ambayo unaweza kupoteza uhalisia wako. Huu ni mfano wa tabia moja ambayo wanawake aina hii hutumia.
#5 Anababaikia kazi unayofanya ama vitu unavyomiliki. Ni kawaida kwa wanawake kubabaikia mambo flani, kwa mfano kama wewe ni daktari basi anaweza kukuona wewe ni mtu muhimu na maana katika maisha kwa kuwa unasaidia wagonjwa. Lakini ukiona mwanamke anakubabaikia ilhali kazi unayoifanya haina maslahi yeyote kwa binadamu, basi atakuwa anafanya hivyo akijua kuwa hio kazi unayofanya inalipa hela nyingi.
#6 Ana ladha ya vitu ghali. Je huyu mwanamke anapenda starehe? Je nguo zake zote ni za designer ana zina nembo tambulika? Je anaweza kujimudu na hizo gharama zote? Kama hawezi basi huyo ni gold digger. Aina hii ya wanawake huwa wanatafuta mwanaume ambaye ana pesa nyingi ili aweze kuyatimiza matamanio yake ambayo yeye mwenyewe hawezi kuyatimiza.
#7 Zawadi zinampoza kama amekasirika. Kiufupi ni kuwa kila wakati ambapo utakosana na yeye ni lazima umpatie zawadi ili aweze kukusamehe. Bila hivyo utabaki na baridi yako.
#8 Hamakiniki na kile unachoongea. Utajua hili kwa kuwa hawezi kukumbuka kile kitu ambacho ulimwambia ama kuongea awali. Hii ni kwa sababu hana upendo wowote kwako, bora pesa tu.
#9 Anasahau siku zako muhimu lakini zake hasahau. Kwa mfano siku muhimu ambazo umepanga mkutane kv kutembelea sehemu flani na wewe anasahau lakini zake kato hawezi. Sehemu zote ambazo amepanga lazima uhurudhurie bila kukosa ama atakufanyia kama ile hatua ya #4 tuliyoiongea awali.
#10 Anataka mhudhurie katika vilabu ama dinner za gharama. Je anapenda gharama ikija katika maswala ya chakula ama klabu? Kama ni kweli basi lengo lake ni kuudondoa mfuko wako. Wanawake gold digger wanapenda kutembelea mikahawa ya gharama hata kama hawana uwezo wa kulipia gharama.
#11 Hujui mambo mengi kumhusu. Je unamjua kiasi gani? Unaijua familia yake? Je anapenda kuongea kuhusu familia yake? Kama haongei basi hii ni dalili ya kuwa analenga mfuko wako.
#12 Hauko ligi moja na yeye. Hebu tuongee ukweli hapa. Huyu mwanamke ni mrembo kuliko wote ushawahi kuwaona. Hujawahi kufikiria kuwa unaweza kumnasua. Lakini ghalfa unamwona ndie huyu. Ukiangalia hali yako ni kuwa hupendeki. Lakini pesa unazo nyingi kupita kiasi. Well, huyu mrembo ni gold digger, usijipe misifa ya bure.
# 13 Anakuomba pesa. Wewe na yeye hamjakuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, labda wiki moja tu lakini huyu mwanamke tayari ashaanza kukuomba pesa bila mpangilio. Shida zote za kwake ameanza kukutajia na anahitaji pesa. Hii ni ishara ya mwanamke gold digger.
# 14 Kazi anayofanya haimpi mshahara wa maana. Kazi anayofanya haimpi mshahara wa maana. Ukichanganya na dalili tulizozieleza hapo juu katika tabia zakee basi bila shaka huyu ni gold digger.
Ok, hapa Nesi Mapenzi huwa hatupendi kuona wanaume wakipoteza muda na wanawake wasiofaa, ushauri wetu ni kuwa ukikumbana ama mpenzi wako anaonyesha dalili za ugold digger tunakushauri leo uweke msimamo wako dhahiri, kama utakubali kusimamiwa akili na mwanamke ama utasimama kama mwanaume alpha na kushika usukani katika mahusiano yako.

Comments
Post a Comment