Wasanii wa Tanzania ni wajinga sana kwenye mikataba – Dudu Baya

Image result for dudu baya
Msanii wa Bongo Flava, Dudu Baya amesema wasanii wengi wa Tanzania wana uwelewa mdogo sana upande wa mikataba.

Dudu Baya amesema kitu hicho kimefanya wawekezaji wengi wakubwa kukimbia katika tasnia muziki kutokana na tabia ya wasanii kupenda kuhama label bila kuzingatia kile walichokubaliana katika mkataba.

“Soko la kumsaini mtu hapa Tanzania ni gumu sana kwa sababu wasanii wa Tanzania ni wajinga sana kwenye mikataba ndio maana hakuna taifa ambalo huwanachoka kwenye tv na redio kusikia fulani amehama label hii, mara nimehama label hii, akikaa kule mwaka mmoja anasema ameibiwa anahamia label nyingine” Dudu Baya ameiambia The Base ya ITV.

“Lakini hawa watu wanaomiliki hizi label ni wavumilivu sana kwa sababu anaangali huyu msanii kakimbia kwenye label mkataba haujaisha anaenda kwenye label nyingine, huyu mtu akienda mahakamani anapoteza muda wake kwa sababu yule msani hata hela ya kumlipa hana” amesema.

Ameongeza kuwa kutokana na tabia hiyo ya wasanii ndio sababu label kama Tetemesha Entertainment, Bongo Records na MJ Records kuacha kusimamia wasanii.

Comments