Mwanamitindo Calisah amesema moja vitu vilivyomuigizia fedha nyingi zaidi kwa mwaka huu, 2017 ni kutangaza biashara ya viatu vya kike ambayo alivivaa kabisa.
Mwanzoni mwa October mwaka huu Calisah aliibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii mara baada ya kuonekana akiwa amevaa viatu hivyo. Akizungumza na Planet Bongo ya EA Radio amesema dili hilo limemuingizia Tsh. Milioni 7.
“Ni moja ya dili iliyoniingizia hela nyingi kwa mwaka 2017, mpaka sasa hivi imevunja rekodi, sijawahi pata dili kama ile hata matangazo niliyokuwa nafanya tofauti tofauti hajafiki kwenye ile amount nimelipwa kwenye vile viatu,” amesema Calisah.
Comments
Post a Comment