Ni Wema na Lulu tayari Jumsuit hii



Hello hello wasomaji wetu wa MSALU TV , leo tunakutana tena katika ulimwengu wa mitindo na kama ilivyo ada yetu kupeana habari na dondo za mitindo zinazofanya vizuri. Na ndio maana leo tunaitazma Jumsuit mpya mjini inayobamba poa.



Nguo hii mpaka sasa imeonekana kuvaliwa na mastaa wawili wa filamu Bongo yaani Wema Sepetu ambaye alivaa katika Instagram Party iliyofanyika nchini Rwanda na hivi karibuni akatinga tena jumsuit kama hiyo katika mitoko yake.



Ila muigizaji Elizabeth Michael’ Lulu’ alitinga kwa mara ya kwanza Jumsuit hiyo katika uzitunzi wa filamu zilizoandaliwa na kituo cha Azam na alipendeza kweli kweli.

Huwenda Jumsuit hizi zimevaliwa pia na mastaa wengine hapa Bongo na nje ya Bongo sema tu! hatuja bahatika kupata picha zao.

Aina hii ya nguo iliyounganisha blauzi na suruali inakuwa na rangi tofauti tofauti kama njano,maua maua yenye mchanganyika wa pinki,zamabara, na rangi zingine zinaonganishwa na suruali ya bwanga nyeusi ambalo hutoa nafasi hata kwa wenye miili mikubwa kuvaa.

Je! wewe kama mdao wa mitindo una jumsuit gani? kabatini kwako?

Comments