Siku 3 ya maandamano mabaya Iran


Haki miliki ya pichaEPAImage captionMmojawepo wa waandamanaji wakikabiliana na Polisi karibu na Chuo Kikuu cha Tehran

Kumeshuhudiwa misururu mibaya ya ghasia kati ya waandamanaji na walinda usalama nchini Iran.

Mikanda ya video iliyowekwa katika mitandao ya kijamii, inaonesha, waandamanaji wawili wakipigwa risasi katika mji wa Dorud- Magharibi mwa taifa hilo.

Huko Ab-har, Kaskazini mwa taifa, waandamanaji waliteketeza bango kubwa iliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

Gari pamoja na pikipiki moja ya polisi, ziliteketezwa moto na waandamanaji huko Mashdad.


Katika mji mkuu Teh-ran, maelfu ya watu waliandamana hadi katika uwanja mmoja wa mkutano, ulioko katikati mwa mji huo, huku wakitoa wito kwa jeshi na polisi kuungana nao.Image captionRamani ya maeneo yaliyoathirika zaidi

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, katika maeneo mengi ya mji mkuu, polisi na makundi ya kiusalama yenye silaha, hawakuonekana kabisa.

Awali, maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono utawala wa nchi hiyo walikuwa na mkutano wao pia.

Katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuhusiana na hali ilivyo nchini Iran, Rais wa Marekani Donald Trump Trump, amesema kuwa utawala wa mataifa yanayokandamiza raia, huwa hayaishi kwa muda mrefu, na kwamba siku itafika wakati ambapo raia wa Iran watafanya maamuzi.Image captionRais wa Marekani Donald Trump

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Iran, imepuuzilia mbali matamshi hayo ya Trump na kutaja kama ni yenye " hila na inayoambatana na udanganyifu".

Mara kwa Mara Marekani imelaani muafaka wa kimataifa uliotiwa saini mwaka 2015, chini ya utawala wa Barrack Obama, kuhusiana na mpango wa kinuklea wa Iran, ili taifa hilo liondolewe vikwazo vya kiuchumi.

Wachanganuzi wanasema kwamba, muafaka huo bado haujaleta manufaa makubwa ya kiuchumi, sawa na alivyoahidi Rais Hassan Rouhani, na huenda ni miongoni mwa yanayochangia maandamano yanayoshuhudiwa kwa sasa, nchini Iran.

Comments