Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amefunguka kwa kudai kwamba mwaka 2017 uliomalizika weekend iliyopita haukuwa mzuri katika muziki wake.
Nay wa Mitego katika muonekano mpya
Rapa huyo ambaye haishiwi matukio, mwaka 2017 aliwekwa ndani na jeshi la polisi kutokana na kuachia wimbo ‘Wapo’ambayo ulidaiwa kuwa maneno ya kutengeneza chuki kwa wananchi na viongozi wao.
“Mwaka 2017 haukua mzuri sanaa. But niseme asante kwa pumzi na afya njema,” aliandika Nay wa Mitego Instagram.
Aliongeza, “Asante mungu kwa Kila Kitu. Asanteni mashabiki wangu ambao mmekua bega kwa bega na mimi kwenye kila jambo ata nilipo kosea hamjawai nitupa, Nawapenda sana. Shukrani kwa media zote kwa support mnayozidi kunipa mungu azidi kuwaongezea mwaka 2018. Happy New Year#NiweDawa,”
Rapa huyo anajipanga kuachia wimbo mpya uitwao, Niwe Dawa.
Comments
Post a Comment