Msanii wa Filamu Bongo, Wema Sepetu amefungua changamoto alizokumbana nazo mwaka jana, 2017.
Muigizaji huyo amesema kwa asilimia kubwa haukuwa mwaka mzuri kwake ila kuna baadhi ya vitu alivyoweza kufanikisha.
“Mwaka 2017 umekuwa ni mwaka mbaya kwangu kuanzia mwezi wa pili tarehe tatu hapo ndipo mwaka wangu ulipoanza kuyumba, nilikuwa sana na msongo wa mawazo na nilikuwa siyo mtu mwenye raha ingawa nilijaribu kutabasamu,” amesema Wema.
Ameongeza kuwa moja vitu alivyofanikisha kwa mwaka huu ni kutoa movie yake ya Heaven Sent ambayo aliiachia katika App yake pekee.
Comments
Post a Comment