Msanii wa muziki nchini Tanzania, Zuwena Mohamed 'Shilole' amefunguka na kusema kuwa amechoshwa na mtu ambaye anajiita na kutumia jina la mume wake Uchebe na kumchafua kwenye mitandao ya kijamii kwa kuweka posti za kumdhalilisha mumewe.
Shilole amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instgram na kudai kuwa Uchebe feki huyo amekuwa akiharibu muonekane wa mume wake kwa jamii kutokana na jumbe mbalimbali ambazo anaziweka kwenye mtandao huo.
"Plzzz plzzz nimechoka na huyo uchebe feki 'walah' ananiharibia muonekano wa mume wangu maana hana maneno haya lol! Mashabiki wangu naomba muipuuze hii acount! Acount ya mume wangu ni @uchebe1 hana fans wala nini" aliandika Shilole
Mbali na Shilole Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Klabu ya Simba SC, Haji Manara pia ameonekana kukerwa na jambo hilo na kusema kuwa anashindwa kuelewa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwanini inashindwa kuchukua hatua kwa watu ambao wanatumia majina ya watu wengine kwenye mitandao ya kijamii na kuwachafua watu kwa kuwa hata yeye pia amekuwa akifanyiwa mchezo kama huo ambao mume wa Shilole Uchebe anafanyiwa.
Comments
Post a Comment